TRAVELER SURVEILLANCE FORM FOR EBOLA SCREENING

Travelers coming to Zanzibar could download and fill in Ebola Surveillance Form before arrival to avoid inconveniences and delays at our points of entry.

Click the link below to download the Form:

EBOLA SURVEILLANCE FORM

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AFUNGUA MKUTANO WA TISA WA TATHMINI YA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa  ya maendeleo katika sekta ya Afya na ipo karibu sana kufikia malengo ya Mellenia.

Amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana ushirikiano wa pamoja wa wafanyakazi wa sekta hiyo na kuimarisha miundo mbinu ya afya ikiwemo ujenzi wa barabara, mawasiliano, umeme na usambazaji wa maji safi.

Balozi Seif ameeleza hayo alipokuwa  akifungua  mkutano wa tisa wa mwaka wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar kwa mwaka uliomalizika katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.

Amesema Zanzibar hivi sasa imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga ambavyo hapo zamani ilikuwa ni tishio kubwa kwa taifa.

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR MAHMOUD THABIT KOMBO AFANYA ZIARA KATIKA VITUO VYA AFYA MKOA WA KASKAZINI ”A” UNGUJA.

MKOKOTONI

Mkuu wa kituo cha Afya cha Mkokotoni Mcha Haji Makame akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (alievaa miwani) alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya afya vya Wilaya Kaskazini A. Wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Ghirmany akifuatiwa na mwakilishi wa UNICEF Zanzibar  Bibi Fransisca.

SERIKALI IMEIMARISHA UTOAJI HUDUMA KWA MAMA WAJAWAZITO

  • Vifo vya watoto vyapungua

SEKTA ya Afya inajukumu kubwa la kusimamia huduma zote za Afya katika visiwa vya Unguja na Pemba, kiwango kizuri cha afya ya watu ndio msingi wa maendeleo ya nchi na jamii kwa ujumla.
Afya ya mwanadamu ni rasilimali pekee ambayo haiwezi kulinganishwa na kitu chochote na kwa maana hiyo kuzingatiwa kwa sekta ya Afya ni jambo muhimu kwa wananchi na wanajamii kwa ujumla.
Baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 hadi kufikia mwaka 1999 Serikali ilikuwa ikitekeleza Sera ya Afya iliyotokana na Ilani ya Chama cha Afro Shirazi Party (ASP) hio ilikuwa ni wakati wa mapambano ya kudai uhuru.

PRESS RELEASE

nemboSTATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

SERIKALI  ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya juhudi  kubwa za kuhakikisha huduma za afya zinaimarika licha ya ongezeko la idadi ya watu hapa  Zanzibar ikilinganishwa na idadi iliyopo kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo mara baada ya kulifungua jengo jipya la upasuaji wa maradhi ya ubongo na  uti wa mgongo lililopo hapo katika hospitali Kuu ya Mnazimmoja mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Shein alisema kuwa kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 idadi ya watu wa Zanzibar ilikuwa  ni laki tatu na ishirini ambapo idadi hiyo imeongezeka mara nne ya wananchi wanaoishi Zanzibar ambao wanafika milioni 1.4 hivi sasa jambo ambalo limepelekea utoaji wa huduma uwe tofauti na mara baada ya Mapinduzi.

Powered by | Designed by: suv | Thanks to trucks, infiniti suv and toyota suv